Je? Wewe ni Mbuzi Kati ya Kundi la Kondoo

Kitakuwa ni kitu cha kushangaza sana endapo mtu ataimbisha wimbo wa mbio za Mwenge kwenye shughuli ya msiba. Au mpishi kuweka sukari kwenye pishi la wali ati. Hii yote ni kwa sababu kila mazingira yana taratibu zake na zikikiukwa basi kunatokea mkanganyiko wa mfumo mzima wa tukio au jamii husika.

Kawaida ni kwamba binaadamu huwezi kuwa katika eneo zaidi ya moja kwa wakati mmoja, ndiyo uhalisia wa mambo. Na kila unapobadili eneo unavaa uhusika wa tabia za eneo hilo, na huu ndio utashi wa binaadamu unaotutofautisha na wanyama pamoja na viumbe wengine.

Ukiwa msibani, utakuwa na utulivu na kufuata taratibu za kuwepo majonzini, ukiwa uwanja wa soka basi utapiga bashasha na kushangilia ipasavyo, ukiingia nyumba ya ibada basi utavaa utulivu na unyenyekevu sawa sawa na mazingira ya ibada.  Vivyo hivyo ukiongea na watoto utakuwa na maneno ambayo yataeleweka kwa watoto hao, na ukibadili nafasi na kuongea na watu wazima zaidi yako utatumia lugha ya staha na kuonyesha heshima kwao. Lakini utakapo kuwa na wenzako, watani wako basi utafanya utani sawia na mazingira ya watu unaotaniana nao. Ukifanya kinyume na haya, basi hali nzima ya uwepo wako inakuwa na mtazamo tofauti na wa taharuki, na kuonekana hufai kwenye eneo la hiyo jamii.

Katika mitandao ya kijamii, tumeona jinsi ambavyo inawezekana kuwepo maeneo mengi kwa wakati mmoja kwa kutumia nguvu ya simu ya mkononi “smart phone”. Una uwezo wa kuwasiliana na makundi kadhaa kwa wakati mmoja, yakijumuisha watu toka nchi mbalimbali na watu wa rika na staha tofauti. Mambo haya yote ni muhimu sana na yana tija pale yanapotumika sawasawa na makusudio yake. Lakini utaratibu unapokiukwa, yanageuka kuwa karaha na kuondoa kabisa ile maana halisi ya lengo la kuundwa kwake.

Mfano, chukulia mtu yupo kwenye kundi la WhatSapp ama Facebook la Alumni wa chuo fulani, watu hawa wanatoka katika maeneo tofauti, wana nyadhifa tofauti, wana imani tofauti nakadhalika. Hapa ni lazima kila mwanakundi atumie utashi wake kuelewa ni mambo ya aina gani yanafaa kuongelewa kwa kundi hili, heshima na staha ikiwa ni kitu cha msingi, na sio heshima kwa wanakundi tu, bali hata wewe kujiheshimisha kwao kwa michango yako na maoni yako. Michango yako ya mawazo, maoni, picha nk Je ina mchango gani jengefu kwenye jamii husika ya hilo kundi? Maana muda ni mali na gharama, hivyo kuchangia mambo yasiyo na tija, ni kupoteza muda wa watu wengine wengi, kambo ambalo sio heshima pia.

Mfano mwingine, inatokea mtu ameingia kwenye kundi lenye madhumuni ya kupeana ushauri nasaha kuhusu kilimo, yeye anashusha picha 100 za biashara yake ya vitenge. Ama kundi la kwaya ya waimbaji fulani wa kidini, halafu mtu anatuma vibonzo vyenye mlengo tofauti kabisa na lengo la kundi.

Mambo haya ni mfano mdogo sana wa jinsi gani watu wengi tunashindwa kufahamu mipaka na malengo halisi ya makundi tunayohusika nayo. Na kwa kufanya hivi, tunapoteza sana tija na umuhimu wa hizi njia za mawasiliano, na kufanya wengine kuona ni upuuzi tu kuhusika na mitandao.

Wenzetu wenye kuelewa mipaka hii, wamekuwa wakitumia makundi haya kujijenga, kusimamia kazi, kuzalisha na hata kupeana ushauri mahsusi katika mambo yao ya msingi na kujijenga kila siku. Makundi na njia hizi za mawasiliano zinatumika kujenga jamii bora, yenye kujitambua na kujikwamua katika maswala mbali mbali yanayohusu maendeleo ya jamii husika. Lakini yote haya yanatokana na uelewa wa mahali, mazingira na maudhui ya kundi na mawasiliano husika.

Mwisho nitoe rai kwa jamii yetu, hasa sisi wageni wa mitandao na teknolojia ya mawasiliano ya kisasa. Kufahamu jinsi gani tunaweza kutumia haya mawasiliano kwa tija, kujijenga na kujikwamua katika maswala mbali mbali. Kufahamu kuwa kutoelewa jinsi ya kuzitumia njia hizi, kuna sababisha madhara makubwa sawia na faida zitokanazo na kufahamu matumizi bora za mawasiliano haya.

Tukijifunza na kuheshimu mipaka na mazingira ya mawasiliano yetu, tutajenga jamii bora, yenye kupanua mawazo, kufurahisha, kustawisha mawasiliano na matokeo yake kuendelea kuwa bora kila siku.

Do You Know what is Social Network?

Na, Je Wafahamu Mipaka ya Huduma za Mtandao?

I know a bit of Swahili so I will do my best to keep up with a few sentences here and there just to keep it live, especially when the message is for my fellows from Tanzania around the world.

There has been a buzz going around amongst Tanzanian political leaders whizzing about moral and what is supposed to be posted on the social network at large, and especially from a few celebrities on the rise.

Kumekuwa na matamshi ya picha za utupu, now this on its own is a very gray area, what does utupu really mean in Tanzanian context? Is a bikini considered utupu? a micro miniskirt? or just pure nude? well, I bet you will be confronted with a variety of definitions and answers from anybody you ask, this is mainly based on their understanding, and fueled by who they are talking about.

The latest was a statement from a minister of art who went ahead and said, “Tume mkamata msanii nyota wa Tanzania ‘Diamond’ kwa kosa la kutuma picha zisizo na maadili mtandaoni, pamoja na msanii mwingine Nandi, lazima wafahamu kuwa mtandaoni sio kokoro la kutupa uchafu wao”

Well here is where I see a problem with the whole fiasco and his or the ministerial office understanding on the matter.

Being on the internet does not mean OPEN, there are several services that are on the internet BUT they are Private.

Anything that has REGISTER then log in to use is not OPEN. Users of these services they have to agree on a set of rules, privacy policies and terms of use in order to qualify to use the services. ONLY if they violate these rules and terms they will be denied use of the system.

Anybody who will in one way or another consume content from these services, should have access to the said services and abide by the rules and regulations of the service. Reading content from Facebook, Instagram, Twitter etc is not open to non-members.

Even within the registered members, you have to FOLLOW or be friends with someone to consume their content.

Hivyo hakuna kitu kama kuvunja maadili mtandaoni tu kwa sababu hazija mpendeza mtu fulani ama muheshimiwa as they call them,  if I am posting content on my account, and the people who have agreed to follow me are using the content.

GOSSIP aka UMBEA

My fellow friends from Tanzania are notorious for gossiping online, they are the best when it comes to scrutinizing somebodies private matters online, they can spread news like wildfire as if they are on commission. This is where the problem begins. This problem has propagated to even the official in high offices, they act very confidently only based on gossip tips if it trends they will trend with it. Wanapiga umbeya kama wanalipwa kwa masaa

They are willing to share photos of dead people, people in an accident, even children doing a different kind of things, it is a pandemic in the society online. For many what matters is somebody gets trashed, taken down, humiliated and shamed. It is sad but that is the reality of things. BECAUSE the inverse if true that, they will not share or spread the news about somebody’s success, or some achievement, or an educative post or something of that nature.

When somebody who uses one system, get an interesting story or a photo of somebody having a good time with the significant other, then they will snap a screenshot, add some comments and then share on a different social network service. That on its own is a breach of privacy and rules of content sharing.

Follow me on these, You read something on Facebook (only registered users can read) you share on Instagram (Only your followers will read, or Instagram registered users) etc. All these services they share a common rule for information sharing. NO CHILD UNDER 13 IS ON THESE networks, or supposed to be. And these services have their international definition of what is considered nude.

When the minister tells the media that inappropriate content has been posted by somebody, the question should be HOW THE HELL DID THE MINISTER GET THE CONTENT? and who actually took the content from the boundaries of the service to the public?

Double Standars
When it comes to online content, it is an ocean to cover, only the trending issues will get condemned, but the rest will continue to soar, this is true even for this issue of maadili mitandaoni. The ministry is focusing only on some individuals and some trending gossip that goes with it, there is no really plan to combat and create an understandable ground rule to guide everybody whether small or big.