Kupenda ni One Way

Kila mtu anapenda anapoangukia kupenda, na akisha penda, basi anaonesha upendo wake wa jinsi yake na namna anavyopenda. 

Lakini mtu anaetokea kupendwa, sio lazima kuwa atakuwa na hali ya upendo sawia na huyo mpenda wake. Na inawezekana kabisa akawa hana upendo kabisa kwa huyo mpenda wake.

Kila mtu anapenda anavyopenda, lakini mara nyingi huwezi kupendwa unavyotaka kupendwa, sababu atakayekupenda, atakuonesha upendo kwa jinsi yake anavyopenda. 

Watu wengi wanataka kupendwa wanavyopenda kupendwa. Bila kufahamu kuwa anaempenda, ana jinsi ya kuonesha upendo wake kwa namna yake.

Inawezekana umefikia maamuzi ya kudhania kuwa hupendwi na unae mpenda, kwa sababu tu, hajakupenda jinsi unavyotaka kupendwa. Ingawa yeye anakupenda kwa dhati na kwa jinsi yake anavyopenda.

Jambo la msingi kufahamu ni kwamba, Kupenda ni ONE WAY, yaani jukumu la kupenda ni suala binafsi, halina ushirikiano. Hivyo ukipenda, basi penda kwa jinsi unavyo penda kupenda. Na usisubirie kupendwa unavyotaka kupendwa.

Ukipenda gauni, ikatokea kipimo chake hakikutoshi, hutalichukia hilo gauni, bali utaendelea kulipenda ingawa huwezi kulivaa sababu halikutoshi.

Ni kawaida sana kupendwa na mtu ambaye huna upendo kwake, ama kupenda mtu ambaye hana upendo kwako. 

Lakini pia mara kadhaa inatokea kupenda mtu anae kupenda, lakini anavyokupenda sivyo unavyopenda kupendwa. Ingawa kila mmoja ana upendo wa dhati.

Na ni aghalabu kupenda mtu anaye kupenda, na akapenda unavyo mpenda na akakupenda unavyopenda kupendwa.

%d bloggers like this: