Unyanyasaji wa Kimtandao “Cyberbullying”

Cyber bullying

“Cyberbullying” Ni uonevu unaotendeka kupitia vifaa vya mawasiliano vya kidigitali, mfano simu, kompyuta, “tablets”, uonevu huu unaweza kutokea kupitis SMS, jumbe fupi za maneno, maandishi ya blogs, program za kwenye simu ama kupitia mitandao ya kijamii, majukwaa nk mahali ambapo watu wanaweza kuhusika kwa kuona, kuandika ama kushea. Uonevu huu unahusisha kutuma, kuandika ama kushirikishana taarifa hasi, za uzushi, uongo au za kuumiza na kudhalilisha kuhusu mtu mwingine ambaye ni mhanga. Inweza husisha kushirikishana taarifa binafsi za mtu binafsi bila hiari yake, na kusababisha aibu, udhalilishaji. Na matendo haya yanapelekea kwenye uvunjifu mkubwa wa makosa ya jinai.

  1. Mahali ambapo mara nyingi uonevu wa kimtandao unafanyika ama kutokea ni:
  2. Mitandao ya kijamii, mfano Facebook, Instagram, Snapchat na Twitter
  3. Jumbe fupi kupitia huduma mbalimbali za simu, Whatsapp, Telegram nk.
  4. Mawasiliano ya barua pepe, blogs nk.

Ulimbukeni wako usihusishe watoto, ama watu wasio na hatia. Tunafahamu kuwa katika jamii yetu kuna wengi ambao tuna ulimbukeni na ujinga wa matumizi chanya ya mitandao ya kijamii. Kiasi kwamba imekuwa na madhara sio tu kwa mjinga mhusika, bali kwa wasiohusika kabisa, na zaidi WATOTO.

Wanaojiita waandishi wa habari wa online TVs na Blogs wamekuwa mstari wa mbele kuishushia heshima tasnia nzima ya habari kwa kukosa miiko wala heshima ya kazi yao. Maslahi ya kupeleka habari za kuvumisha zenye uzushi yamewekwa juu, kuliko ubora wa habari kwa jamii. Hii imepelekea kwamba kila mahojiano, yana lengo la kuchokonoa maisha binafsi, mambo ya kuabisha na kuchochea ugonvi, yote haya kwa lengo la kuuza.

Ni matumaini yangu kuwa, jamii yetu itaendelea kuelimika na kukataa kushiriki katika kunyanyasa watoto, na watu wasio na hatia kupitia mitandao ya kijamii na taarifa za kimtandao. Kila mmoja anaweza punguza tatizo hili kwa kuto shirikisha “share” taarifa ama habari yoyoteyenye unyanyasi wa aina yoyote.

Habari ikikosa wasomaji, itakosa soko, hivyo tunaosababisha habari za kiunyanyasaji kuwa nyingi ni sisi ambao tunashinda mitandaoni kuzisoma, ku-share na kutoa maoni ya uchochezi.

Taarifa yoyote inayoingia kwenye mtandao, ni ya kudumu, itakuwepo mpaka uzee wa mwenye taarifa. Hivyo ujinga wa leo ndio utakuwa sababu kubwa ya kumsababisha mwanao akose nafasi katika maisha yake kwa sababu ya historia ya yaliyopo mitandaoni juu yake.

Tutambue kuwa kama jamii, kwa ujumla wetu kila mmoja ana jukumu kubwa kuhakikisha ustawi bora wa jamii yetu, heshima kwa jamii yetu, taifa letu na utu wetu. Kuna fahari sana katika kushirikishana mambo chanya yenye kujenga jamii, kuelimisha, kuongeza mshikamano na pia heshima kitaifa. Watoto wetu tuwalinde na kuwakuza katika jamii yenye kuwalea kwa upendo na kuwapa uwezo wa kutengeneza maisha yao kwa jinsi wanavyoweza. Tupeane maonyo na kufundishana lakini tuepuke kudhalilishana, mmoja akidhalilika, jamii inadhalilika.

Kwa pamoja tuwe na kampeni ya makusudi, kupunguza na kuondoa kabisa mitandao ya kijamii ambayo lengo lake kuu ni kusambaza taarifa za kudhalilisha watu, kushambulia wasio na hatia, kuchonganisha kwa lengo la kujiingizia kipato. Unapotembelea mitandao hiyo, ndivyo unavyowaingizia kipato na kuwawezesha kuendeleza madhara haya, hivyo UKIEPUKANA na kusoma, kutembelea ama kushea mitandao iliyo na malengo kama haya, utasaidia pia kuwafanya waangalie upya misingi yao na malengo ya huduma zao kwa jamii.

Niwatakie utumiaji wa mitandao ya kijamii wenye TIJA kwa jamii yetu na watoto wetu.

%d bloggers like this: