Utakapo fanikiwa kutofautisha na kutenganisha maisha yako na mafanikio yako ya hali na mali. Utaishi maisha kamilifu na yenye kusudi. Na utakuwa mtu mwenye furaha ambayo itakuletea mafanikio.
Kupenda ni One Way
Kupenda ni “one way,” ni suala binafsi, halina ushirikiano…
Ukimpenda mtu, ni wewe umependa, haijalishi kama unapendwa nae ama la. Hivyo wewe penda unae mpenda na unavyotaka kupenda. Na usitake kupendwa unavyopenda, maana kila mtu anapenda anavyopenda na anapopenda.
Unyanyasaji wa Kimtandao “Cyberbullying”
“Cyberbullying” Ni uonevu unaotendeka kupitia vifaa vya mawasiliano vya kidigitali, mfano simu, kompyuta, “tablets”, uonevu huu unaweza kutokea kupitis SMS, jumbe fupi za maneno, maandishi ya blogs, program za kwenye simu ama kupitia mitandao ya kijamii, majukwaa nk mahali ambapo watu wanaweza kuhusika kwa kuona, kuandika ama kushea. Uonevu huu unahusisha kutuma, kuandika ama kushirikishana […]
Je? Wewe ni Mbuzi Kati ya Kundi la Kondoo
Je hujawahi kuona mtu anaingizwa kwenye grupu la wanasheria halafu anashusha picha 200 za biashara yake ya nguo toka china? ama mtu anaingia kwenye grupu la kikundi cha kwaya halafu anatuma picha za “kanga moko”? hawa ni wengi wetu ambao hawafahamu mipaka na mazingira ya mawasiliano mitandaoni. Wanaweza imbisha wimbo wa Mwenge kwenye msiba. Ungana na mwandishi wa makala hii kupata kufahamu mazingira na matumizi bora ya mawasiliano ya tehama, na changamoto katika jamii yetu.